Text: | Kama ulivyoagiza |
Author: | J. Montgomery |
1 Kama ulivyoagiza
kabla kuuawa,
hivi nitafanya Bwana,
nitakukumbuka.
2 Wewe kwa ajili yangu
ulitoa mwili,
katika mkate wako huu,
nitaukumbuka.
3 Vivyo damu ya thamani
wewe ulitoa.
Katika kikombe hiki
nitaikubuka.
4 Nitazamapo Golgota,
kuona msalaba,
na kipaji cha kafara
nitakikumbuka.
5 Siwezi kusahau jinsi
ulivyoumia,
kweli nikiwapo mzima
nitakukumbuka.
6 Kwa hiyo nakungojea
ee Bwana, kwa kuwa
ujapo mara ya pili,
utanikumbuka.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Kama ulivyoagiza |
Title: | Kama ulivyoagiza |
English Title: | According to Thy gracious word |
Author: | J. Montgomery (1825) |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Chakula cha Bwana |
Notes: | Sauti: Martyrdom by H. Wilson, Lutheran Book of wotship #98, Service Book and Hymnal #486, Hymnal Companion #323 |