234. Ukae kwetu Bwana

1 Ukae kwetu Bwana
na rehema yako,
shetani asiweze
kutudhuru tena.

2 Ukae kwetu Yesu
na neno la kweli,
tupate ukombozi
tukilifuata.

3 Ukae kwetu nuru
na mwanga wa mbingu,
utuongoze njia
iendayo kwako.

4 Ukae kwetu Bwana
mwenye enzi yote,
utupe nguvu nyingi
tukutumikie.

5 Ukae kwetu Mponya
na nguvu yako kuu,
adui na dunia
wasituharibu.

6 Ukae kwetu Mungu
na ukweli wakio.
tusikache wewe.
Utupeleke juu!

Text Information
First Line: Ukae kwetu Bwana
Title: Ukae kwetu Bwana
German Title: Ach bleib mit deiner Gnade
Author: J. Stegmann, 1588-1632
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Sikukuu za Wakristo
Notes: Sauti: Ach bleib mit deiner Gnade, Namba 198, Posaunen Buch, Erster Band #7, Nyimbo za Kikristo #186
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us