243. Kristo usituondoke

1 Kristo usituondoke
sababu mchana waisha,
mwanga wa Neno la Mungu
usiuzimishe kwetu!

2 Nyakati hizi za mwisho
tusaidie kushika
neno la huruma yako
nalo fumbo takatifu.

3 Kundi lako ulilinde
ulikusanye mwenyewe,
libariki neno lako,
litangaziwe popote!

4 Mambo na mashauri yote
si yetu ila ni yako,
kwa hiyo wasimamishe
wanaokutegemea.

5 Neno lako ngome kubwa,
hata boma la makundi:
kwa neno lako tulishe,
tusitafute mengine!

Text Information
First Line: Kristo usituondoke
Title: Kristo usituondoke
German Title: Ach bleib bei uns, Herr Jesu Christ
Author: N. Selnecker, 1532 (1530)-1592
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Sikukuu za Wakristo
Notes: Sauti: Herr Jesu Christ, dich zu uns wend, Asili: Görlitz 1648, Posaunen Buch, Erster Band #20
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us