63. Yesu Mwokozi

1 Yesu Mwokozi
mwenye nguvu zote,
wewe Mwana wa Mungu
Nitakupenda, nitakusifu,
uliye mpenzi wangu mkuu.

2 Uzuri wote
wa nchi na milima
unatufurahisha.
Yesu ni mzuri kupita hiyo
anatufariji sisi.

3 Jua na mwezi
hata nyota zote
zinang'aa mbinguni.
Yesu ashinda uzuri huo,
ang'aza watu mioyo.

4 Uzuri wote
hapa a mbinguni
ni mfano wa Mwokozi.
Tumpende yeye wa utukufu
aliyetupenda kwanza.

Text Information
First Line: Yesu Mwokozi
Title: Yesu Mwokozi
German Title: Schönster Herr Jesu
Author: Hajulikani
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Source: Münster, 1677
Notes: Sauti: Kijerumani, Asili: Silesia, 1842, Posaunen Buch, Erster Band #254, Augustana Hymnal #317, Lutheran Book of Worship #518
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us