15. Tawi limechipuka

1 Tawi limechipuka
shinani mwa Yese,
kama tulivyopashwa
habari na wazee.
Likatoa ua
wakati wa usiku lilipochanua.

2 Isaya alitaja
ua hilo zuri.
Ni Yesu, mponya wetu,
Maria alimzaa
usiku mtulivu.
Uwezo wake Mungu,
umefanya hivi.

3 Na ua hili dogo
lanuka vizuri;
lang'aa kama jua
giza lafukuzwa.
Ni Mwana wa Mungu,
hata mwana Adamu;
Mwokozi wa watu.

4 Siku ya kufa kwetu
Yesu tuongoze,
tuiache dunia,
twende furahani
mbinguni kwa Mungu.
Pale tutakusifu
Pasipo kukoma.

Text Information
First Line: Tawi limechipuka
Title: Tawi limechipuka
German Title: Es ist ein Ros' entsprungen
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Notes: Sauti na wimbo: Es ist ein Ros' entsprungen, Asili: Kön 1599, Posaunen Buch, Erster Band #228, Lutheran Book of Worship #58
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us