Text: | Nakushukuru Mungu |
Author: | Georg Niege, 1525-1583 |
1 Nakushukuru Mungu
kwa kinywa na moyo
saa hii ya asubuhi
hata siku nzima.
Nitakuimbia,
nitakusifu Baba,
alivyonifundisha
Mwanao wa pekee.
2 Umenilinda Bwana,
usiku kucha huu
ukaondoa shida,
hatari na msiba.
Nakuomba sasa:
Uondoe makosa
niliyokukosea
kwa neno na tendo.
3 Nilinde hata leo
kwa neema yako tu,
asinishinde mwovu
kwa hila yake kuu.
Nisione shida
ya moto na ya maji,
ya homa na ugonjwa,
ya kufa kubaya.
4 Mungu atanitunza
aliye Mwenyezi,
ayabariki yote
nitakayotenda.
Namwekea yeye
uzima hata kufa,
anitendee yale
yanayompendeza.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Nakushukuru Mungu |
Title: | Nakushukuru Mungu |
German Title: | Aus meines Herzens Grunde |
Author: | Georg Niege, 1525-1583 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Nyimbo za asubuhi |
Notes: | Sauti: Aus meines Herzens Grunde, Asili: David Wolder, Hamburg, 1598, Posaunen Buch, Erster Band #5 and #94 |