263. Njooni tuimbe wimbo huu

1 Njooni tuimbe wimbo huu:
Atupenda!
Mungu ni mwenye huruma!
Atupenda!
Mliolala amkeni,
mumtafuteni Mwokozi!
Woga wa kufa uishe!
Atupenda!
Atupenda! Atupenda!
Njooni tuimbe wimbo huu!
Atupenda!

2 Utume mewema ndio huu:
Atupenda!
Alitujia toka juu,
atupenda!
Mwanawe Mungu, Mwokozi
atuita sote: Njooni!
Mlioshindwa na mwovu,
atupenda!
Atupenda! Atupenda!
Njooni tuimbe wimbo huu!
Atupenda!

3 Ametufia Golgota,
atupenda!
Katupatia uzima,
atupenda!
Mponya ni jua la watu,
Yeye ni ngao vitani.
Tumtafuteni kwa bidii,
Atupenda!
Atupenda! Atupenda!
Njooni tuimbe wimbo huu!
Atupenda!

4 Majaribuni atufaa,
atupenda!
Atukaribisha kwake,
atupenda!
Yeye ni mfalme na shujaa.
Yeye hachoki kulinda
watu wote wamwombao,
atupenda!
Atupenda! Atupenda!
Njooni tuimbe wimbo huu!
Atupenda!

Text Information
First Line: Njooni tuimbe wimbo huu
Title: Njooni tuimbe wimbo huu
German Title: Kommt, stimmet alle jubelnd ein
Author: E. Gebhardt, 1832-1899
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu
Notes: Sauti: Kommt, stimmet alle by E. S. Lorenz, 1854, Reichs Lieder #30, Nyimbo za Kikristo #211
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us