66. Nyesha mvua

1 Nyesha mvua, nyesha mvua,
wewe Roho wa Baba,
nchi kavu ikanyweshwe,
imsifu Mungu wetu!

2 Vuma sana, vuma sana,
Roho mwenye uzima,
tulio na usingizi
utuamshe kwa mkono!

3 Toa mwanga, toa mwanga,
Roho kwani unang'aa
wewe ushinde usiku
tusikae na giza.

4 Sikiliza, sikiliza,
wewe mfalme wa mbingu!
Tuma Roho wako kwetu,
kote kuwe na upya!

Text Information
First Line: Nyesha mvua, nyesha mvua
Title: Nyesha mvua
German Title: Geist vom Vater, taue taue
Author: R. Amstein, 1846-1923
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Epifania, Mission
Notes: Sauti: Stille senkt der duft'ge Schleier by F. A. Schulz, 1842, Reichs Lieder #323, Nyimbo za Kikristo #53
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us