Go Ad-Free
If you regularly use Hymnary.org, you might benefit from eliminating ads. Consider buying a Hymnary Pro subscription.
Text: | Useme Nami Bwana |
1 Useme nami Bwana, uninong'oneze,
Useme na upendo kwamba sitaachwa;
Uufungue moyo ili nisikie,
Unijaze na sifa nikushangilie
Refrain:
Useme nami Bwana, useme na pendo,
Nitakuwa mshindi kwa uweza wako;
Useme kila siku, nitakusikia,
Useme nami Bwana, kwamba sitaachwa.
2 Useme nasi Bwana, kwako tuongozwe,
Tujazwe na furaha na utufundishe;
Tujitoe uzima kwa Ufalme wako,
Mbinguni kwa milele, tukuone humo. {Refrain]
3 Kama ulivyosema na watu wa kale,
Useme nasi sasa, Neno litendeke;
Nikutukuze Bwana, siku zangu zote,
Nikuheshimu pia, sasa na milele. [Refraom]
Text Information | |
---|---|
First Line: | Useme nami Bwana |
Title: | Useme Nami Bwana |
Refrain First Line: | Usame nami Bwana |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1994 |
Scripture: | |
Topic: | Ushuhuda; Wokovu |
Notes: | Sauti: Sepak to my Soul, Lord Jesus, Redemption Songs #567 |