1 Karibu kwangu Roho
ingia moyoni,
uliyeniletea uzima na raha.
Roho Mtakatifu
wa Baba na wa Mwana
ufananaye nao
ukaaye nao.
2 Unafundish watu
kuomba vizuri,
wapate kusikiwa
na Mungu mbinguni.
Unatuombea,
hukomi, mpaka Mungu
atende mambo yale
uliyoyaomba.
3 Wafurahisha moyo,
hupendi huzuni;
tukiwa matesoni,
unatutuliza.
Wazungumza nasi
Kwa neno lko tamu,
unatia mioyo
furaha ya kweli.
4 Unatufanya sisi
kuwa usharika;
hutaki tugombane
na kuchukiana.
Wanaopigana
unawapatanisha;
wataka wapendane
Wakristo wowote.
5 Umlinde Rais wetu,
serikali yetu,
tukae na amani
duniani humu.
Uwape wakubwa,
pamoja na wadogo
uchaji na akili,
wampendeze Mungu.
6 Katika mwendo wetu
utupe na sisi
nguvu, tumshinde mwovu
akitujaribu.
Utusaidie,
tushike njia yako
na mwisho tufe vema
tufike kwa Mungu.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #126