1 Mungu ndiye Mwamba wetu, nguvu za milele;
Hatuogopi kwa kuwa twapatana naye.
Refrain:
Kabla ya kuumba vyote dunia na vitu,
Wewe, Mungu, ulikuwa Mungu wa milele.
2 Wewe hutumainiwa zamani na leo.
Nguvu zako zawatosha watu wako, Bwana. [Refrain]
3 Kwako, Wewe miaka elfu ni kama kitambo,
Mbingu zijapotoweka, Wewe utadumu. [Refrain]
4 Mungu ndiye Mwamba wetu, nguvu za milele,
Twakunyenyekea Wewe, Twakutumaini [Refrain]
Source: Nyimbo Za Imani Yetu #14