Text: | Mfalme wa upendo ndiye |
Author: | H. W. Baker, 1821-1877 |
1 Mfalme wa upendo ndiye
anichungaye mimi,
yeye ni wangu milele,
ananipenda daima.
2 Kando ya maji uzima
hunipeleka mimi
katika malisho mema,
anilisha siku zote.
3 Mara nyingi napotea
kwa ukaidi wangu,
naye ananitafuta,
na kunirudisha kwake.
4 Kivuli cha kufa kwangu
sitaogopa Bwana,
ukiwa kwangu daima
masaka wayaondoa.
5 Wanitandikia meza,
naula mkate wako,
nanywa katika kikombe
nikumbuke kufa kwako.
6 Siku zangu zote hapa
wema wako u vivyo.
Nikubali Mchunga mwema,
nikuimbie milele.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Mfalme wa upendo ndiye |
Title: | Mfalme wa upendo ndiye |
English Title: | The king of love |
Author: | H. W. Baker, 1821-1877 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Chakula cha Bwana |
Notes: | Sauti: Dominus regit me by J. B. Dykes, 1832-1867, Service Book and Hymnal #530 |