Text: | Kuna nchi nzuri |
Author: | A. Young |
1 Kuna nchi nzuri mbali sana.
Wako watu wema, wasimama,
waimba vizuri sifa zake Mwokozi,
nasi duniani twamtukuza.
2 Njooni kwa nchi hii njooni sasa!
Mbona mwasimama mashakani?
Tuache makosa, yanamchukiza Bwana,
Kwake tutaketi kwa salama.
3 Machozi hapana, wala hamu,
mbele yake Baba mapenzi tu.
Utaona raha utapewa kilemba
kuvikwa na wale wa mbinguni!
Text Information | |
---|---|
First Line: | Kuna nchi nzuri |
Title: | Kuna nchi nzuri |
English Title: | There is a happy land |
Author: | A. Young |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kufa na kuzikwa |
Notes: | Sauti: Happy land, Asili: Amerika, Hymnal Companion #512 |