Text: | Babangu kule mbinguni |
Author: | H. Bone |
1 Babangu kule mbinguni,
aliye juu pa malaika,
aangalia njia zangu
na kunilinda maisha,
aangalia njia zangu
na kunilinda maisha.
2 Hata unywele kichwani
hauanguki ovyo tu
na siri zote za moyoni
zajulikana kwa Baba,
na siri zote za moyoni
zajulikana kwa Baba.
3 Zamani nisipojua,
amekwisha kuandika
mokononi mwake jina langu,
ndio upendo wake mkuu,
mokononi mwake jina langu,
ndio upendo wake mkuu,
4 Ee Baba yangu u mwema,
nami nataka kufanya
kama malaika wafanyavyo
mbinguni kwako milele!
kama malaika wafanyavyo
mbinguni kwako milele!
Text Information | |
---|---|
First Line: | Babangu kule mbinguni |
Title: | Babangu kule mbinguni |
German Title: | Mein Vater, der im Himmel wohnt |
Author: | H. Bone |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Nyimbo za asubuhi |
Notes: | Sauti: Steh' ich in finstrer Mitternacht, Asili: Kijerumani, Tumwimbie Bwana #25, Nyimbo za Kikristo #167 |