253. Ninataka kumwimbia Muntu

1 Ninataka kumwimbia
Mungu kwa furaha kuu.
Ninaona kila siku
anihurumiavyo.
Moyo wake mwenye kweli
umejaa upendo tu,
abariki kwa wingi
wamtumikiao vema.
Vitu vyote vyaisha,
pendo lake milele.

2 Kama kuku alindavyo
watoto hatarini,
vivyo Baba anilinda
kila siku kwa nguvu.
Ndiye aliyeniumba
akanipa mwili huu
na uzima na roho
siku zote mpaka leo.
Vitu vyote vyaisha,
pendo lake milele.

3 Jinsi hii aliupenda
Mungu ulimwengu huu,
hata akamtoa mwana,
kwa ajili ya watu.
Naye Yesu aliteswa
akafa kule mtini
atuokoe sisi.
Tazameni pendo hili!
Vitu vyote vyaisha,
pendo lake milele.

4 Roho wake mtakatifu
ni kiongozi wangu,
aniangalia vema
niingie mbinguni,
Aning'aza moyo wangu
kwa tegemeo langu
limshindalo Shetani,
asiweze kunidhuru.
Vitu vyote vyaisha,
pendo lake milele.

5 Nikishikwa na huzuni
ninajue faraja:
Shida na mateso yote
mwisho yatageuka.
Baada ya kaskazi kali
yanakuja masika
vivyo baada ya shida
napewa furaha kubwa.
Vitu vyote vyaisha,
pendo lake milele.

6 Pendo lake haliishi
Neno hili ni kweli.
Basi mimi mtoto wake
ninamwomba Babangu:
Unihurumie mimi,
nikushike kwa nia,
nikupende daima,
niishipo duniani;
na halafu milele
nitakaa na wewe.

Text Information
First Line: Ninataka kumwimbia
Title: Ninataka kumwimbia Muntu
German Title: Sollt ich menem Gott nicht singen
Author: P. Gerhardt, 1607-1676
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu
Notes: Sauti: Lasset uns den Herren preisen by J. Schop, 1641, Posaunen Buch, Erster Band #56, Nyimbo za Kikristo #201
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us