| Text: | Mjini kwake Babangu |
| Author: | Mch. Sila Msangi |
1 Mjini kwake Babangu
Ndipo pa raha
Tutafika juu kwake
Tukae naye.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Lini tutafika kwake
Tuungane na malaika
Mjini kwake, mjini kwake.
2 Pale kwake Babngu
Ndipo pazuri
Siku ile kuu mno
Ya kupaona.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Mji ung'arao mno
Ni makao ya maliaka
Mjini kwake, mjini kwake.
3 Nikipanda mlimani
Na kuyaona
Yote ya utukufu
Aliyofanya.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Yote yanisimulia
Ufahari wake Baba
Mjini kwake, mjini kwake.
4 Njoo mwenzangu tazama
Yote ya Mungu
Yote ameyafanya
Kwa ajili yetu
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Tuinue macho yetu
Tumtazame mwumba wetu
Mjini kwake, mjini kwake.
| Text Information | |
|---|---|
| First Line: | Mjini kwake Babngu |
| Title: | Mjini kwake Babangu |
| Author: | Mch. Sila Msangi |
| Refrain First Line: | Kuna raha Kuna raha |
| Language: | Swahili |
| Publication Date: | 1988 |
| Topic: | Kujuta na kutegemea: Kutegemea |