1 Mjini kwake Babangu
Ndipo pa raha
Tutafika juu kwake
Tukae naye.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Lini tutafika kwake
Tuungane na malaika
Mjini kwake, mjini kwake.
2 Pale kwake Babngu
Ndipo pazuri
Siku ile kuu mno
Ya kupaona.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Mji ung'arao mno
Ni makao ya maliaka
Mjini kwake, mjini kwake.
3 Nikipanda mlimani
Na kuyaona
Yote ya utukufu
Aliyofanya.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Yote yanisimulia
Ufahari wake Baba
Mjini kwake, mjini kwake.
4 Njoo mwenzangu tazama
Yote ya Mungu
Yote ameyafanya
Kwa ajili yetu
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Tuinue macho yetu
Tumtazame mwumba wetu
Mjini kwake, mjini kwake.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #321