49. Twapenda ukaapo

1 Twapenda ukaapo
Bwana wetu enzini,
furaha zako wewe
zinazipita zote.

2 Palipo pa kuomba
wajapo watu wako
na wewe Bwana upo,
uwakubali wote.

3 Twapenda neno lako,
habari za wokovu,
za nguvu za kushinda,
za shangwe za mbinguni.

4 Twapenda nyimbo zako,
tunaziimba hapa,
mpaka tutaziimba
pamoja na malaika.

5 Utujalie Yesu,
tuzidi kukupenda,
tuone uso wako
utakavyotakata.

Text Information
First Line: Twapenda ukaapo
Title: Twapenda ukaapo
Author: Hajulikani
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Mwaka Mpya
Notes: Sauti: Nun lasst uns Gott dem Herren by N. Selnecker, 1587, Sauti: Nyimbo za Kikristo #39
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us