56. Nani mpenzi wangu mkuu?

1 Nani mpenzi wangu mkuu?
Nani ninayemsifu?
Nani ninayemjua?
Nani ninayempenda?
Ndiye Yesu Mwokozi.
Ndiye Yesu Mwokozi.

2 Nani nimtegemee,
anipaye moyo mkuu?
Nani aondoaye
makosa, shida zangu?
Ndiye Yesu Mwokozi.
Ndiye Yesu Mwokozi.

3 Nani anayenipa
nguvu nyingi za roho?
Nani anifanyaye
mwenye haki kwa Mungu.
Ndiye Yesu Mwokozi.
Ndiye Yesu Mwokozi.

4 Nani mwenye faraja,
nikiona huzuni?
Nani atulizaye
moyo wenye taabu?
Ndiye Yesu Mwokozi.
Ndiye Yesu Mwokozi.

5 Nani azishindaye
hata nguvu za kufa?
Nani anipeleke
baadaye kwake Mungu?
Ndiye Yesu Mwokozi.
Ndiye Yesu Mwokozi.

Text Information
First Line: Nani mpenzi wangu mkuu?
Title: Nani mpenzi wangu mkuu?
English Title: Wollt ihr wissen, was mein Preis?
Author: J. C. Schwedler, 1672-1730
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Epifania, Mission
Notes: Sauti: Wollt ihr wissen, was mien Preis, Grosse Missionsharfe, Erster Band #78, Reichs Lieder #95, Nyimbo za Kikristo #43
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us