87. Nataka kusimama

1 Nataka kusimama
chini ya msalaba,
kama kivuli cha mwamba
wakati wa mchana,
kama ni maji nyikani,
kambi safarini,
na hapa nitapumzika,
kwani jua kali.

2 Mahali pema sana
chini ya msalaba,
kwani hapo waoneka
upendo wa Yesu.
Yakobo alivyoona
ndotoni zamani,
mti Yesu aliowambwa,
ni ngazi kwa Mungu.

3 Juu ya msalaba huo
Yesu alikufa.
Alikufa tuokoke,
tuliopotea.
Ninastaajabu kabisa
ni mambo mawili:
kwake Yesu ni upendo,
kwangu mimi kosa!

4 Wataka kuonana
na Yesu mbinguni,
yakupasa kukaa kwanza
chini ya mti huo.
Ni kweli siku chache tu
mateso na shaka.
Halafu pasipo mwisho
furaha kwa Bwana!

Text Information
First Line: Nataka kusimama
Title: Nataka kusimama
English Title: Beneath the cross of Jesus
Author: E. C. Clephane, 1830-1869
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuteswa na kufa kwa Yesu
Notes: Sauti: Beneath the cross of Jesus by C. D. Sankey, 1840-1908 and F. C. Maker 1844-1927, Reichs Lieder #263, Lutheran Book of Worship #107
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us