Go Ad-Free
If you regularly use Hymnary.org, you might benefit from eliminating ads. Consider buying a subscription.
Text: | Watu Wa Yesu |
1 Watu wa Yesu, sifuni Bwana,
M-tangazeni, ulimwenguni,
Sifa za Yesu, zienee pote,
Mataifa yote, yamsifu Yesu.
2 Humilki pote, mbingu na n-chi,
Ufalme wake, hauna mwisho,
Wote wa mbinguni m-tukuzeni,
Msifuni daima hata milele.
3 Neema yake ni nyingi sana,
Upendo wake ni wa ajabu,
M-linzi, M-chunga,Mwokozi wetu
Mfarifi, Mwombezi na Kiongozi.
4 Fadhili zake zaonekana,
Anavikidhi viumbe vyake,
Vyakula, vinywaji ni vingi kwake,
Mwangaza na mvua atugawia.
5 Sifuni Bwana kamwimbieni,
Anastahili fahari yoge,
Heshima na pendo m-peni Bwana,
Mwokozi Mwombezi na Mfalme Yesu.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Watu wa Yesu, sifuni Bwana |
Title: | Watu Wa Yesu |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1994 |
Scripture: | |
Topic: | Irada, Sifa Na Injil |
Notes: | Sauti: O Worship the King (Lyons), Baptist Hymnal 1991 #16, Nyimbo za Sifa #1, Milo wa Ab- Magipo 3/4 |