Hymnal: Nyimbo Za Imani Yetu #163 (1994) Topics: Maisha Ya Kikirsto Na Uhuduma First Line: Kazi yake Mungu Baba Refrain First Line: Na Yeye Lyrics: 1 Kazi yake Mungu Baba
imewekwa kwetu.
Kazi yake Mungu Baba
imewekwa kwetu.
Tangu Mwanzo wa Mitume
hadi hivi sasa.
Tangu Mwanzo wa Mitume
hadi hivi sasa.
Refrain:
Na Yeye
Katuagiza
Kasema
Kwa Mamlaka
Aliyo
Pewa na Baba
Nendeni
Duniani pote.
Hubirini kwa Jina la Baba,
Mwana, Roho, watu waokoke.
Hubirini kwa Jina la Baba,
Mwana Roho watu waokoke.
2 Mataifa wana njaa
ya Neno la Mungu.
Mataifa wana njaa
ya Neno la Mungu.
Nayo kiu ya milele
imewakalia.
Nayo kiu ya milele
imewakalia. [Refrain]
3 Hivyo ndugu tutimize
wajibu wa Bwana.
Hivyo ndugu tutimize
wajibu wa Bwana.
Ili siku ikifika
tutoe hesabu.
Ili siku ikifika
tutoe hesabu.[Refrain]
Scripture: Matthew 28:19-20 Languages: Swahili
Kazi Yake Mungu Baba