![Text Text](https://hymnary.org/sites/hymnary.org/themes/newhymn/icons/20x20/page-text.png)
Hymnal: Mwimbieni Bwana #196 (1988) First Line: Ukimpata mwenye moyo Lyrics: 1 Ukimpata mwenye moyo
Mwaminifu daima,
Umepata kito bora,
Wajaliwa na Mungu
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
2 Ukiingiwa na taabu
Na kupatwa na msiba,
Mwenzi wako mwaminifu
Atakutia moyo.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
3 Haja yake mwenzi huyu
Kukusaidia tu.
Taabu yako ndiyo yake,
Hakuachi msibani.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
4 Rafiki za duniani,
Mali zitapotea,
Mwenzi wako mwaminifu
Atakaa kwa mpenziwe.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
5 Mtu kuwa na mwenzake
Mwaminifu daima,
Ndiyo hali duniani
Ipitayo kabisa.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri. Languages: Swahili
Ukimpata mwenye moyo mwaminifu