1 Haleluya, Haleluya, Mwokozi Kafufuka Haleluya, haleluya. Kweli alituahidi kuwa atafufuka. Haleluya, haleluya.
Refrain: Duniani ni amani, Juu mbinguni ni utukufu, Duniani ni amani, Juu mbinguni ni utukufu.
2 Siku mbili kaburini, ya tatu kafufuka. Haleluya, haleluya. Ni dalili ya kushinda, mauti imshindwa. Haleluya, haleluya. [Refrain]
3 Sasa uzima tele kwa kila aaminiye. Haleluya, haleluya. Tusihofu twende hima atatupa uzima. Haleluya, haleluya. [Refrain]
Source: Nyimbo Za Imani Yetu #91