1 Mwamba wenye imara,
Kwako nitajificha.
Maji na damu yako,
Toka mbavuni mwako,
Iwe dawa ya kosa,
Kutakasa mioyo.
2 Si kazi za mikono,
Ziletazo wokovu.
Nikitoa machozi,
Nikifanya kwa bidii,
Siwezi kujiosha,
Unioshe wewe tu.
3 Sina la mikononi,
Naja msalabani.
Ni uchi, nipe nguo,
Dhaifu, nipe nguvu,
Niondolee taka,
Nitakase sijafa.
4 Nikaapo dunia,
Nifikapo kifoni.
Nitakapofufuka,
Nitakapokuona,
Mwamba wangu wa kale,
Kwako nitajificha.
Source: The Cyber Hymnal #15523