1 Yesu mponya tu hapa,
moyo watulia,
mawazo yetu yote
uyavute kwako.
Mwanga wa neno lako,
utuangaze wote,
tuwe na mwangazo.
2 Kaa karibu na sisi,
tunakutamani,
mfunzi wetu ni wewe,
sisi wanafunzi.
Nenolo lia nguvu,
litatufanya wapya,
laongoza vema.
3 Tuna furaha kubwa,
tunakungojea.
Wewe u mwamba wetu
tutegemeao.
Bwana tunakushika
mpaka tunapofika
uzimani kwako.
4 Twataka utufunze
kuwa na upole.
Tufanane na wewe
ujipunguzayo
utimizavyo kazi
ulivyofanya bidii
kuwa mpatanishi.
5 Nguvu ya roho yako
ionyeshe kwetu,
unavyomulikia
wanaopotea.
Kwa kinywa chako Yesu
utushinde na sisi,
tuwe wako kweli!
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #47