Text: | Namwandama Bwana |
1 Namwandama Bwana
kwa alilonena,
Njia yangu huning'azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.
Refrain:
Amini utii
njia pekee ni hii
Ya furaha kwa Yesu:
amini ukatii.
2 Giza sina kwangu
wala hata wingu.
Yeye mara huviondoa
Woga, wasiwasi,
sononeko, basi;
Huamini natii pia. [Refrain]
3 Masumbuko yote,
sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki,
vivyo hubariki.
Niamini nitii pia. [Refrain]
4 Mimi sitajua
raha sawasawa
Ila yote Yesu anipa;
Napata fadhili
na radhi kamili,
Niamini nitii pia. [Refrain]
5 Nitamfurahia
na kumtumaini,
Safarini hata nyumbani;
Agizo natenda;
nikitumwa huenda,
Huamini natii pia. [Refrain]
Text Information | |
---|---|
First Line: | Namwandama Bwana |
Title: | Namwandama Bwana |
English Title: | When we walk with the Lord |
Refrain First Line: | Amini utii |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Sikukuu za Wakristo |
Notes: | Sauti: When we walk with the Lord, L.S. #211, Sacred Songs and Solos #542, R.S. #495 |