266. Baba yetu aliye mbinguni

1 Baba yetu aliye mbinguni
amenifurahisha kwa kweli.
Kaniambia rohoni mwangu
Yesu yu nami, ananipenda.

Refrain:
Anipenda Yesu Mwokozi,
anipenda, anipenda.
Anipenda Yesu Mwokozi,
anipenda kweli.

2 Nimwachapo nikaenda mbali,
yeye ye vivyo ananipenda.
Akaniita kwake upesi,
Yesu yu name, ananipenda. [Refrain]

3 Ananipenda nami nampenda,
wokovu wangu ulipokuja.
Tukimwona kufani Golgota,
Yesu yu nami, ananipenda. [Refrain]

4 Kujua haya kwanipa raha,
kumtegemea kuna furaha.
Amfukuzapo hivi Shetani,
Yesu yu nami, ananipenda. [Refrain]

5 Sifa ni nyingi asifiwazo,
moja ni kubwa katika hizo.
Hata mbinguni nitamwimbia
Yesu yu nami ananipenda! [Refrain]

Text Information
First Line: Baba yetu aliye mbinguni
Title: Baba yetu aliye mbinguni
English Title: I am so glad that our father
Author: P. B. Bliss
Refrain First Line: Anipenda Yesu Mwokozi
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu
Notes: Sauti: I am so glad that our father by P. B. Bliss, Redemption Hymnal #570, Reichs Lieder #217, Nyimbo za Kikristo #214
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us