210. Tuombee Wakristo Duniani

1 Tuombee Wakristo
duniani,
Wasiache ahadi
za imani.

Refrain:
Ee Bwana,
Utujaze Roho Wako;
Ee Bwana,
Utujaze mioyoni.

2 Tuombee wakuu
wa Kanisa,
Wanaolitangaza
Neno lako. [Refrain]

3 Hata na watawala
wetu wote,
Ili tuzidi kuwa
na amani. [Refrain]

4 Ee Bwana, uwe nao
mataifa,
Wakubali Injili
ya wokovu. [Refrain]

5 Tuwaombee wote
waje Kwako,
Wapate kukusifu
siku zote. [Refrain]

Text Information
First Line: Tuombee Wakristo
Title: Tuombee Wakristo Duniani
Author: Francis Ntiruka
Refrain First Line: Ee Bwana, Utujaze Roho Wako
Language: Swahili
Publication Date: 1994
Scripture:
Topic: Maombi
Notes: Sauti ya Kirundi, Tufurahi na Kuimba #29
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us