1 Uamke kwetu tena Roho
ya mashahidi wale wa kwanza,
waliokesha siku zote,
waliomshinda yule adui,
wakihubiri neno la Yesu
kwa watu wa ulimwengu wote.
2 Uwashe moto wa upendo,
uendelee pote kuwaka.
Peleka watu mavunoni,
wanaofanya kazi kwa bidii.
Bwana mwenye mavuno, tazama:
Watenda kazi yako ni haba.
3 Mwanao ametuaqiza
kuomba hivi kwa jina lake,
na sisi wanafunzi wake,
twashika neno lake kwa bidii.
Twaomba hivi kwa moyo wote.
Ee Bwana usikie, ufanye!
4 Utame watu wengi sana,
walitangazi neno kwa nguvu.
Usaidie tuokoe,
ufalme wa Shetani uishe.
Usimamishe, Bwana wa mbingu,
ufalme wako ulimwenguni!
5 Uteme mwema na uende
mahali popote huku nchini,
wamizimu na waingie
kundini mwako mwa wateule.
Amsha nao Waisraeli
na Waislamu waje, wakutii.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Uamke kwetu tena Roho |
Title: | Uamke kwetu tena Roho |
German Title: | Wach auf, du Geist der ersten Zeugen |
Author: | K. H. v. Bogatzky, 1690-1774 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Epifania, Mission |
Notes: | Sauti: I. G. Riemeyer, 1704, Posaunen Buch, Erster Band #8, Lutheran Book of Worship #382 |