47. Yesu mponya tu hapa

1 Yesu mponya tu hapa,
moyo watulia,
mawazo yetu yote
uyavute kwako.
Mwanga wa neno lako,
utuangaze wote,
tuwe na mwangazo.

2 Kaa karibu na sisi,
tunakutamani,
mfunzi wetu ni wewe,
sisi wanafunzi.
Nenolo lia nguvu,
litatufanya wapya,
laongoza vema.

3 Tuna furaha kubwa,
tunakungojea.
Wewe u mwamba wetu
tutegemeao.
Bwana tunakushika
mpaka tunapofika
uzimani kwako.

4 Twataka utufunze
kuwa na upole.
Tufanane na wewe
ujipunguzayo
utimizavyo kazi
ulivyofanya bidii
kuwa mpatanishi.

5 Nguvu ya roho yako
ionyeshe kwetu,
unavyomulikia
wanaopotea.
Kwa kinywa chako Yesu
utushinde na sisi,
tuwe wako kweli!

Text Information
First Line: Yesu mponya tu hapa
Title: Yesu mponya tu hapa
German Title: Treuer Heiland, Wir sind hier
Alterer: Chr. H. Zeiler, 1779-1860
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Mwaka Mpya
Notes: Sauti na wimba: Treuer Heiland, Wir sind hier by K. Kocher (DIX), Stuttgart, 1838, Reichs Lieder #16, Nyimbo za Kikristo #37
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us