1 Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Refrain:
Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.
2 Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu Mwanawe Mungu. [Refrain]
3 Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu. [Refrain]
4 Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi,
’Tapita humo kwa damu. [Refrain]
5 Nitaketi na Yesu huko milele,
Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu Mwanawe Mungu. [Refrain]
Source: The Cyber Hymnal #15524