| 15523 | The Cyber Hymnal#15524 | 15525 |
| Text: | Tangu Siku Hijo Aliponijia |
| Author: | Rufus Henry McDaniel |
| Translator: | Unknown |
| Tune: | [Tangu siku hiyo aliponijia] |
| Composer: | Charles Hutchinson Gabriel |
| Media: | MIDI file |
1 Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Refrain:
Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.
2 Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu Mwanawe Mungu. [Refrain]
3 Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu. [Refrain]
4 Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi,
’Tapita humo kwa damu. [Refrain]
5 Nitaketi na Yesu huko milele,
Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu Mwanawe Mungu. [Refrain]
| Text Information | |
|---|---|
| First Line: | Tangu siku hiyo aliponijia |
| Title: | Tangu Siku Hijo Aliponijia |
| English Title: | What a wonderful change in my life has been wrought |
| Author: | Rufus Henry McDaniel |
| Translator: | Unknown |
| Refrain First Line: | Amani moyoni mwangu |
| Language: | Swahili |
| Copyright: | Public Domain |
| Tune Information | |
|---|---|
| Name: | [Tangu siku hiyo aliponijia] |
| Composer: | Charles Hutchinson Gabriel |
| Key: | A Major |
| Copyright: | Public Domain |