5. Nikulakije vema

1 Nikulakije vema
Bwana wangu Yesu?
Wote wanakungoja
wapewe uzima.
Nuru yako ing’aze
hata moyo wangu,
nijue mambo mema
yakupendezayo.

2 Wamekutandikia
maua na nguo.
Nami nakuimbia
nyimbo za furaha.
Moyo ukupendeze
kwa sifa na nyimbo,
ukakutumikie
siku zangu zote.

3 Umetoka mbinguni
ukawa maskini.
Ukaacha furaha
utupe uzima.
Na tuliponyang’anywa
ufalme na raha,
ukaja mponya wetu
kuturudishia.

4 Nalifungwa na mwovu,
ukanifungua.
Nikawa nimetwezwa,
ukanifanya,
Ukanifanya mkubwa,
ukanipa mali,
zisizomalizika
kwa kutu na wezi.

5 Umenijia mimi
sababu ya nini?
Sababu ya kupenda,
uwaponye wote
waonao huzuni
kwa makosa yao.
Wakijuta kwa kweli
utawapokea.

6 Ushike neno hili,
Umati wa Yesu,
ukiwa na huzuni
na shida popote.
Usiogope kitu:
wokovu tayari.
Anayetufariji
yu karibu sasa.

Text Information
First Line: Nikulakije vema
Title: Nikulakije vema
German Title: Wie soll ich dich empfangen
Author: Paul Gerhardt, 1607-1676
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Yesu anangojewa
Notes: Sauti: Valet will ich dir geben by M. Teschner, 1613; Wimbo: Posaunen Buch Erster Band #59, Melodienbuch #8, Nyimbo za Kikristo #5, Service Book and Hymnal #11
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us